Waziri wa Nishati, January Makamba amesema kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, megawati 50 zinazozalishwa kutokana na umeme wa jua zitaingizwa katika Gridi ya Taifa.
Waziri Makamba amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, TANESCO itaingiza megawati hizo ikiwa ni historia kwa taifa ambapo haijawahi kutokea kwa umeme wa jua kuingizwa katika Gridi ya Taifa.
Ameongeza kuwa Mradi huo unagharimu kiasi cha Euro milioni 43 sawa na shilingi bilioni 109.65 huku awamu ya pili ikihusisha ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 100 utakaogharimu kiasi cha Euro milioni 72.30 sawa na shilingi bilioni 184.37.