Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Megawati 15 za umeme wa gesi kuanza kuzalishwa

9e47ecfc64989b116fee6b164d79b81a Megawati 15 za umeme wa gesi kuanza kuzalishwa

Tue, 23 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMPUNI ya Shema Power Lake Kivu (SPLK) inatarajia kuzalisha megawati 15 za umeme kufikia Juni mwaka huu ikiwa ni awamu ya kwanza ya kutumia gesi ya methane kutoka Ziwa Kivu.

Umeme huo unatarajiwa kuongeza megawati 56 katika gridi ya taifa, huku serikali ikiwa imewekeza dola za Marekani milioni 400 katika uchimbaji wa gesi ya methane.

Mradi huo ulioanza Oktoba, 2019 unatarajiwa kukamilika Desemba, 2022 na kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme nchini.

Meneja wa REG katika wilaya ya Rubavu, Laurent Butera alisema awamu ya kwanza ya mradi huo itasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa umeme katika wilaya hiyo ambayo ni ya kimkakati kwa biashara ya Rwanda katika kusaka soko la DRC.

Wilaya ya Rubavu inakuwa ya kwanza kunufaika na mtambo huo wa gesi ya methane ambapo kwa sasa inatumia umeme kati ya megawati saba na 10.

Licha ya mikakati ya kutumika kibiashara, wilaya hiyo itasambaza nishati hiyo katika wilaya za Musanze na Karongi.

Kampuni ya Shema Power Lake Kivu (SPLK) inafanya kazi na kampuni ya Rwanda Energy Group (REG) kutekeleza mradi huo kwa kasi.

Mhandisi wa SPLK, Laurent Sibomana alisema wanajenga awamu hiyo ya majaribio itakayotoa mwanga wa kuendelea kwa awamu nyingine kwani wanachimba gesi katika kina cha mita 300 mpaka 450 chini ya maji. "Kwanza tunatenganisha gesi na maji, halafu gesi tofauti na methane ambayo hutumiwa kutoa nishati," alisema.

Sibomana alisema nishati inayozalishwa katika mtambo huo wa gesi utahamishiwa kituo cha umeme cha REG ambacho kimeunganishwa na gridi ya taifa.

Asilimia 74 ya kaya katika mji wa Rubavu zimeunganishwa na umeme, lakini wakazi wanasema bado kuna changamoto zinazohusiana na usambazaji wa nishati hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz