Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchengerwa atoa maagizo ujenzi soko la Bukoba

Mchengerwa Kuwasilisha Kwa Rais Majina Ya Viongozi Wanaojihusisha Na Siasa Mchengerwa atoa maagizo ujenzi soko la Bukoba

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ametoa maagizo kwa uongozi wa Mkoa wa Kagera na Manispaa ya Bukoba kuhakikisha hawakwamishi utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Soko la kisasa utakaoanza kutekelezwa kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.

Ametoa maagizo hayo alipotembelea soko kuu la wafanyabiashara wa Manispaa ya Bukoba na kuwahakikishia kuwa kupitia Mradi wa uboreshaji wa miundombinu mbinu ya Miji ya Tanzania (TACTIC) kwa miji 15 kundi la pili Bukoba wanaenda kunufaika na soko la kisasa lenye hadhi ya kimataifa kama la Kariakoo Dar es salaam.

Amesema ili mradi huo uweze kutekelezwa haraka uongozi wa Manispaa ya Bukoba na Mkoa wa Kagera wanapaswa kujiandaa kuanzia sasa na kuandaa eneo zuri la wafanyabiashara kuhamia ili kuendelea kufanya biashara zao na kulipa kodi wakati utekelezaji ukiendelea.

"Tunaweza kupata mkandarasi haraka ,fedha haraka lakini mradi ukakwamishwa na kutojipanga ,naomba kuanzia sasa tujue wapi wafanyabiashara wanahamia kabla ya mradi kuanza kutekelezwa,biashara haipaswi kusimama ,kodi ziendelee kulipwa huku mradi wa soko ukiendelea kukamilishwa sitegemei ukwamishaji wala malalamiko "amesema Mchengerwa.

Amesema kuwa mradi huo uzingatie kuwapitia maeneo wafanyabiashara wote walionyanganywa maeneo sokoni kipindi cha Nyuma,wafanyabiashara wapya,waliopo ,wanaopanga bidhaa nje ya soko na wote wapate nafasi katika soko jipya litakalojengwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live