Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchanga sasa kuanza kusafirishwa saa 24

Mchanga 1 Uchimbaji Mchanga

Wed, 15 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Filbeto Sanga, amesema kuwa utaratibu wa kusafirisha mchanga kwa saa 24 unaandaliwa.

Amesema baada ya maandalizi kukamilika, wataruhusiwa kusafirisha kwa saa 24 badala ya muda wa sasa wa saa 12.

Sanga aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wadau wa mchanga, ambao wanachimba mchanga katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

"Utaratibu umeishaandaliwa na mkuu wa mkoa wa Pwani, wa kusafirisha mchanga saa 24, badala ya saa 12," alisema.Aliongeza kuwa kusitishwa kusafirisha mchanga kwa saa 24 kulitokana na ajali iliyotokea mwaka juzi na kuua watu 14 wa familia moja.

Alisema Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, atatoa kibali siku yoyote kuanzia sasa ambacho kitawaruhusu wadau wa mchanga kusafirisha kwa saa 24.

Sanga akiongeza kuwa pamoja na kuruhusiwa kusafirisha mchanga, wenye magari watatakiwa kuwaajiri madereva wenye sifa kwa ajili ya shughuli hiyo.

Alisema kutokana na kusafirisha mchanga kwa saa 24 wamiliki wa malori wanatakiwa kuajiri madereva wawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live