Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchakato wa kulipwa walioweka fedha benki ya FBME waiva

FEDHA Mchakato wa kulipwa walioweka fedha benki ya FBME waiva

Mon, 8 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Bodi ya Bima ya Amana Tanzania, Isack Kiwili amesema tayari mchakato wa kuwalipa waliokua wateja wa benki ya FBME umekamilika kwa asilimia kubwa na siku chache zijazo wananchi waliokua wameweka fedha zao kwenye benki hiyo wataanza kulipwa.

Kiwili aliyasema hayo Mei 5, 2023 visiwani Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) zilizopo kinazini mjini Unguja.

Amesema mchakato huo wa malipo kwa wananchi walioweka fedha zao kwenye benki hiyo iliyofungiwa nchini mwaka 2017 ulikwama kwa sababu mbalimbali za kisheria.

‘’Shida ni kwamba watu hawajui sisi tulikua na uwezo wa kuzuia kwa hatua ya awali kutokana na madai ambayo tulipokea kwa wenzetu lakini hatukua na uwezo wa kuwagawia wateja fedha zao kwasababu sheria isingeweza kuturuhusu kufanya hivyo,’’aliongezea.

Akitaja idadi ya fedha ambazo wateja wote Nchini Tanzania waliozoweka kwenye benki hiyo. Mkurugenzi huyo alisema kwa upande wa Tanzania bara Sh12.7 trilioni ziliwekwa na kwa upande wa Zanzibar Sh20.5 trilioni ziliwekwa na madai ya wateja wa nje ya Nchi Sh308.2 trilioni

Kiwili amesema kwa hatua ya wali wateja watalipwa nusu ya kile walichokiweka huku hatua nyingine zaidi za kumaliza malipo yao zikiendelea kufanyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live