Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

McDonald's yatangaza kuondoka Urusi

Mc Donalds'.jpeg McDonald’s

Thu, 19 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya McDonald’s imetangaza kuondoka Urusi moja kwa moja. Kampuni hiyo ilifungua mgahawa wake wa kwanza jijini Moscow miaka 30 iliyopita. Baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, kampuni hiyo ililazimika kufunga kwa muda migahawa yake zaidi ya 800 nchini humo.

McDonald’s imenukuliwa ikisema kuwa ” mgogoro wa kiubinadamu unaosababishwa na vita ya Ukraine na mazingira ya biashara ambayo hayatabiriki zimepelekea kampuni yetu kuona kuwa kuendelea kumiliki biashara Urusi hakutaweza kudumu na wala sio jambo thabiti kwa maadili ya kampuni.”

Mkurugenzi mkuu wa McDonald’s nchini Urusi Chris Kempczinski amesema kuwa anajivunia sana wafanyakazi zaidi ya 60,000 ambao wamekuwa wakifanya kazi na kampuni hiyo nchini humo na kuwa uamuzi wa kufunga kabisa biashara ulikuwa mgumu sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live