Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge atoa ushauri matumizi makini Stempu za Kielektroniki

76492 Pic+stempu

Fri, 20 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Wakati Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiendelea na awamu ya pili ya mfumo wa stempi za kielektoniki, Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu amesema suala la matumizi ya stempu hizo haliwezi kuwa na tija ikiwa taasisi mbili hazitakaa pamoja na kutengeneza mkakati.

Komu alisema katika kulisaidia taifa kwenye makusanyo ya ushuru na kodi, ni vyema TRA na Shirika la Viwango nchini (TBS) wakakaa pamoja na kuweka mkakati wa jinsi ya kufanya ili kufikia mafanikio.

Mbunge huyo alisema licha ya Tanzania kuingia katika stempu za kielekroniki kwa bidhaa zake ikiwemo vinywaji, lakini wadau nao hawatakiwi kuwa mbali katika mchakato huo kwani kila kunapokucha nao wanaongeza teknolojia.

Hata hivyo alisema, wengi wa watu ambao wanagushi si Watanzania bali ni watu wanaotoka mataifa mengine ambao kwao teknolojia imekuwa kwa kiasi cha hali ya juu lakini akahoji ni kwa nini wataalamu wanashindwa kuzipa ubora bidhaa za Tanzania.

“Ni jambo jema kufikia huko, lakini TRA na TBS wasipokuwa wamoja hatuwezi kumaliza tatizo, unajua TRA anatengeneza stempu wakati mwenzake anazikagua sasa hapa katikati lazima kuwepo na elimu ya kutosha kwa watu ili wajue ipi halali na ipi imegushiwa,” alisema Komu.

Mbunge huyo alisema watu wengi wamekuwa wakinyweshwa pombe ambazo si halali na hata zikiwa halali nyingi huwa hazilipiwi kodi jambo alilosema kwa duania ya sasa halipaswi kuwepo.

Pia Soma

Advertisement
Naye Naibu Waziri wa Viwanda na  Biashara, Stella Manyanya alilieleza Mwananchi kuwa vita hiyo ilikuwa ni kubwa kwasababu ilikuwa ikifanywa na watu wenye fedha, lakini akaahidi kupambana hadi Serikali ifanikiwe.

Aidha, mfumo huo kwa sasa upo katika awamu ya pili, kuanzia Agosti Mosi Mwaka huu, Mamlaka ya mapato nchini (TRA) ilitangaza kuanza kutumia mfumo huo kwa bidhaa za vinywaji baridi kama soda na vinginevyo visivyo na kilevi, Vile ambavyo vimekwisha ingizwa sokoni vitauzwa kama kawaida hadi Januari 31 mwaka 2020.

Awamu ya kwanza ya mfumo huo unaosimamiwa na Kampuni ya Uswis iitwayo Societe Indusrielle et Commerciale de Produits Alimentaires (SICPA), iliyoanza januari 15 mwaka huu ilikuwa ni kwa vinywaji aina ya bia, Mvinyo na pombe kali.

Aidha Juni mwaka huu Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo aliliambia Mwananchi kuwa takwimu zinaonyesha kuna ongezeko la ukusanyaji wa mapato kutokana na awamu ya kwanza ya mfumo huo.

“Tuna imani mfumo huu utaongeza mapato, kwa awamu ya kwanza tu, tumefanikia kuongeza mapato ya ushuru wa forodha kutoka Sh24 bilioni kwa Januari hadi Sh28 bilioni Aprili,” alisema mpaka wakati huo mashine 44 za ETS zilikuwa zimefungwa katika viwanda mbalimbali

“Mfumo huu unarahisisha upatikanaji wa hesabu halisi za uzalishaji na malipo ya ushuru wa forodha bila kuingiliwa na mtu, tuliwiwa kufanya kazi naSICPA  baada ya kuona mafanikio ya mfumo huu katika nchi za Kenya, Morocco, Uganda, Malaysia, Brazil, Turkey na Albana,” alisema.

Alisema sasa TRA inakuwa na uwezo wa kujua kiwango halisi kinachozalishwa na punde Mamlaka hiyo itazindua programu ya simu ambayo itamuwezesha mteja kujua kama bidhaa hiyo ina stempu ya TRA.

Chanzo: mwananchi.co.tz