Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ataka masharti sawa maduka ya kubadilisha fedha

50667 Pic+mbunge

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Baraza la Wawakilishi (CCM) Jaku Hashim Ayub ameitaka Serikali kuweka masharti yenye uwiano katika biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni.

Ameyasema hayo leo Ijumaa Aprili 05, 2019 wakati akichangia makadirio na mapato ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Amesema mambo mengi Tanzania Bara yameigwa kutoka Zanzibar na kwamba amesikia kuwa fomula ya maduka itakuwa ngumu.

“Zanzibar ni ndogo inategemea sana utalii na kwamba muangalie masharti yaliyopo yawe na uwiano. Zanzibar inategemea utalii na watalii watapata shida. Fomula itasokota sana wananchi,” amesema.

Mbunge huyo pia ameomba kuangaliwa upya kwa utaratibu unaotumika katika mgawanyo wa fedha kutokana na utaratibu wa kuipa Zanzibar asilimia 4.5 ya pato kuwa ni ya muda mrefu.

Jaku pia ameomba kuangaliwa upya kwa suala la mgawanyo wa ajira kwa sababu suala hilo limekuwa gumu.

Pia amelalamikia viongozi maarufu wanaofika nchini kuishia Tanzania bara lakini wamekuwa hawaitembelei Zanzibar.



Chanzo: mwananchi.co.tz