Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ataka mapitio nauli za ATCL

ATCL ATCL CARGO TATU.jpeg Mbunge ataka mapitio nauli za ATCL

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti Maalum, Asha Abdallah Juma amehoji bungeni ni lini serikali itafanya mapitio ya bei ya nauli za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema kwa kawaida nauli za safari za ndege hupangwa na soko kulingana na aina ya huduma inayotolewa.

‘’ATCL kama ilivyo kwa mashirika mengine ya ndege yanayotoa huduma zake kibiashara, nauli zake zinapangwa na soko kwa kuzingatia matakwa ya sheria za ushindani, ambapo vigezo vinavyotumika katika kupanga nauli hizo ni pamoja na gharama za uendeshaji, ili kuhakikisha kuwa mashirika ya ndege yanahimili ushindani wa soko na kujiendesha kwa tija na ufanisi, ‘’ amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live