Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge asisitiza ubunifu kwa utalii

UTALII NZURI 0 Mbunge asisitiza ubunifu kwa utalii

Sun, 11 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Aliyasema hayo jana katika hafla ya uzinduzi wa upishi wa pizza ndefu Tanzania yenye urefu mita 10 iliyopikwa na Hoteli ya Park Hyatt kupitia mgahawa wa Beach House, Shangani Mjini Unguja.

Alisema upishi huo umewavutia wageni wengi waliopo katika mgahawa huo ambao umechangia hoteli hiyo kuongeza kipato.

“Ubunifu kama huu ni jambo zuri sana unachangia kuutangaza utalii wa Zanzibar na kama unavyoona leo (jana) hapa watu wamejaa kushuhudia uzinduzi wa upishi huu wa piza ndefu,” alisema.

Turky alisema katika kukuza utalii, hakuna kuridhika watalii kutembelea vivutio vya utalii pekee bali kuwa na ubunifu wa ziada ili kupata faida zaidi.

Mbunge huyo alizitaka hoteli zingine kuwa wabunifu ili kuwavutia watalii kwa sababu watalii wanapenda kuona vitu vipya ambavyo nchini kwao havipo.

Naye Meneja wa Park Hyatt Zanzibar, Nicolas Cedro, alisema lengo la kuandaa upishi huo ni kukuza utalii wa Zanzibar na kuwavutia wageni wanaofika Zanzibar.

Alisema kuwa upishi huo wa piza ndefu umewakutanisha watu wa mataifa mbalimbali kujionea na kula chakula hicho ambacho kimenogeshwa na viungo vya  Zanzibar.

Baadhi ya wageni waliofika katika mgahawa huo, walisema  upishi huo wa piza ndefu ni mara ya kwanza kuuona na umewavutia sana.

Chanzo: ippmedia.com