Mbunge wa Mtwara Mjini, Hassan Mtenga ameishauri Serikali kuachana na makandarasi zaidi ya mmoja katika ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutokana na umuhimu wa reli hiyo kwa usalama wa Taifa.
Mtenga ameyasema hayo jana jumatano Juni 22,2023 wakati akichangia mjadala wa bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2022/2023.
Amesema katika ujenzi wa reli ya Tazara walijenga raia wa China na reli ya kati walijenga Wajerumani hadi mwisho hakukuwa na ubadilishaji wa mkandarasi.
“Naiomba Serikali kwenye dhana ya usalama wa nchi, hebu turudi sasa tuangalie ni mkandarasi gani bora ambaye anaweza kuingia joint venture na kampuni nyingine wakajenga reli hii,” amesema.