Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge alia na utaratibu GGML

Katambiz Mbunge alia na utaratibu GGML

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MBUNGE wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu amehoji bungeni kama serikali inatambua utaratibu wa Mgodi wa GGML kuwafungia vijana ambao waliwahi kupata changamoto mgodini mwao wasiweze kupata ajira mgodi wowote nchini.

Akijibu swali hilo leo Septemba 8, 2023, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi amesema serikali imewahi kupata malalamiko kuhusu Mgodi wa GGML ku-blacklist vijana ambao wamesitishiwa ajira zao na mgodi huo kwa sababu mbalimbali.

Hata hivyo amesema ufuatiliaji uliofanyika haukubaini suala hilo na kilichobainika ni kuwa Mgodi umeweka utaratibu wa kutunza taarifa za kiutendaji na mienendo ya wafanyakazi wake ikiwemo matendo/matukio ya ukiukwaji wa kanuni na taratibu ambayo mfanyakazi anakuwa amefanya katika kipindi cha ajira yake.

“Katika utaratibu wa kuajiri, kampuni/waajiri karibu wote hufuatilia taarifa za utendaji wa waombaji wa kazi kwa waajiri wao wa awali,” amesema Naibu Waziri.

Amesema GGML imekuwa ikitoa taarifa za utendaji na mienendo ya wafanyakazi waliowahi kufanya kazi nao pale inapoombwa kufanya hivyo na kwamba pamoja na kutoa taarifa hizo, GGML haizuii kwa namna yoyote mgodi husika kuwaajiri waombaji.

“Nitumie fursa hii kuwataka vijana ambao wana uhakika utumishi wao katika Mgodi wa GGML haukuwa na dosari na wanaweza kuthibitisha kuwa wamekuwa black-listed katika Kampuni hiyo kuwasiliana na Ofsi yangu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa,” amesema Naibu Waziri.

Katika swali lake la nyongeza Mbunge huyo amesema ana ushahidi wa suala hilo na pia kuhoji kama ni sahihi mhusika kuadhibiwa milele asiajiriwe sehemu nyingine, ambapo Naibu Waziri amemtaka ampatie ushahidi huo ili aufanyie kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live