Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge alia na bei ya uchimbaji visima

Kisima Cha Majiii Mbunge alia na bei ya uchimbaji visima

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Lupa Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya Masache Kasaka ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maji, kupunguza gharama za uchimbaji wa visima ili mitambo ya uchimbaji ilivyosambazwa mikoani iweze kuwasaidia wananchi.

Masache ameliambia Mwananchi Digital leo Jumatano Novemba 8, 2023 muda mfupi baada ya kuhoji swali kwa Wizara ya Maji, ambapo alitaka kujua ni lini Serikali itatoa mwongozo wa kupunguza gharama za uchimbaji wa visima.

“Tunatambua Serikali ina nia njema kuzogeza huduma ya maji kwa jamii lakini kuna baadhi ya taasisi wameshindwa kupata huduma hususan jimboni kwangu kufuatia gharama kubwa,” amesema.

Masache amesema ni vyema Serikali kupitia Wizara husika ikaandaa mwongozo ambao utasaidia kupunguza gharama za huduma hiyo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi amesema gharama hizo ni kutokana na ubora wa kazi lakini pia wataalam, urefu wa vipimo na ufanisi mkubwa unaofanywa kupitia mradi huo.

“Unaweza kuona gharama ya Sh20 milioni ni kubwa kwa sababu ni pesa lakini ukienda kwa kampuni ya mtu binafsi atakuchimbia kwa Sh5 milioni lakini baada ya muda kutakuwepo na malalamiko,” amesema Mahundi.

Kwa upande mwingine Mahundi, amesema kama Wizara watakaa kuangalia namna ya kupunguza gharama kwani lengo la Rais Samia Sululu Hassan kusambaza magari nchi nzima ni kuona kila mmoja ananufaika na huduma ya maji safi na salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live