Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ahoji ujenzi bandari ya Bagamoyo, Serikali yamjibu

52959 BANDARI+PIC

Thu, 18 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema bado haijaingia mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani hivyo utekelezaji wake haujaanza.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Aprili 18,2019 bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Magogoni (CUF),  Suleiman Ally Yusufu.

Katika swali la nyongeza mbunge huyo amesema mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kati ya Serikali na Oman umekuwa kikwazo cha Oman kusaidia ujenzi wa bandari ya Mpigaduli.

Kwenye swali la msingi mbunge huyo anahoji Serikali ya Muungano inaungaje mkono nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kujenga bandari kubwa.

Akijibu, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Sima amesema Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimeendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali ya uendelezaji wa bandari nchini.

Amesema Serikali ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikiunga mkono nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kujenga bandari kubwa ili kuimarisha miundombinu na huduma za bandari.



Chanzo: mwananchi.co.tz