Mbunge wa Bunda, Mwita Getere amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba kutoa taarifa wamekusanya kiasi gani cha fedha zinazotozwa kutokana na miamala ya simu na kodi za majengo.
Akichangia bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2022/223 jana Jumanne Juni 22,2022, Getere amesema awali wakati Waziri Ummy Mwalimu akiwa waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) alikuwa akitangaza fedha zinazopatikana kutokana na miamala ya simu.
Amesema alikuwa akitangaza fedha hizo zimekwenda katika miradi gani ya huduma za jamii lakini hivi sasa hazitangazwi tena.
“Tunataka kufahamu kiasi cha fedha zilizokusanywa kutokana na miamala ya simu na majengo,” amesema Getere.