Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ahoji bei ya sukari kuwa juu

16652 Pic+sukari TanzaniaWeb

Tue, 11 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Lubeleje ameihoji Serikali kwanini wananchi waendelee kusumbuka kutokana na bei ya sukari kuwa juu wakati bidhaa hiyo imejaa katika maghala viwandani.

Lubeleje alitoa kauli hiyo bungeni leo baada ya kuomba mwongozo kwa Spika kuhusu bei ya sukari kuwa juu ambapo inauzwa kati ya Sh2,600 hadi Sh3000 kwa kilo wakti imejaa katika maghala ya viwanda.

“Nilikuwa naangalia TV jana kwenye maghala hadi juu kabisa viwandani imejaa. Kama kuna kosa la jinai na kuna kesi ya mtu kuingiza sukari sasa wananchi waendelee kusumbuka hadi kesi iishe?” alihoji.

Akijibu, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya alisema ni kweli kumekuwa na ongezeko la bei ya sukari katika baadhi ya mikoa.

“Hakuna bei elekezi iliyotolewa ila natarajia bei ya sukari ni ile ambayo imetoa gharama za uzalishaji, lakini natambua kuna mbinu za wadau kuingiza bidhaa hiyo nchini bila kufuata taratibu husika,” alisema na kuongeza:

“Lengo la Serikali ni kuona bidhaa zinazouzwa nchini zinauzwa kwa bei halali iwezekanavyo. Tumefanya hivyo katika maeneo mengine na sukari ni eneo tunalifanyia kazi. Na tutaleta mrejesho hapa bungeni,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz