Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Toufiq akomalia ujenzi kiwanda cha mafuta

Mafuta Ya Kula Mbunge Toufiq akomalia ujenzi kiwanda cha mafuta

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti Maalumu, Fatuma Toufiq amehoji Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha mafuta ya kula yanazalishwa nchini kwa wingi.

Leo Ijumaa Septemba Mosi, 2023 mbunge huyo amehoji namna gani Serikali itawasaidia wakulima wa mazao yanayozalisha mafuta ya kula ili waongeze uzalishaji zaidi.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kutekeleza mkakati wa kuendeleza sekta ndogo ya Alizeti na Chikichi ambayo ndiyo mazao makubwa yanayoweza kuzalisha kwa tija mafuta ya kula hapa nchini.

Naibu Waziri amesema katika utekelezaji wa mkakati huo, viwanda vipya, kama

Qstec na Jeolong vimeanzishwa ikiwemo upanuzi wa viwanda kama Mount Meru Millers.

Amesema Serikali imeongeza nguvu katika Taasisi za utafiti wa mbegu na hivyo kuongeza uzalishaji wa mbegu bora za alizeti na michikichi.

Kigahe amesema kwa sasa serikali imeelekeza nguvu zaidi kwenye kilimo cha kuzalisha mbegu bora ili kukidhi mahitaji ya malighafi katika viwanda vya ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live