Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbolea kuanzia kilo 5 yaanza kuuzwa madukani

IMG 4385 Hussein Bashe.jpeg Mbolea kuanzia kilo 5 yaanza kuuzwa madukani

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kwa sasa mbolea imeanza kufungashwa kwa ujazo tofauti na inapatikana madukani.

Akijibu swali Bungeni jijini Dodoma Bashe amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya Serikali kutambua mahitaji ya mbolea kwa Wakulima yanatofautiana na kwamba uhitaji wa mbolea kwa ajili ya mazao ya bustani ni kwa kiasi kidogo kulinganisha na mazao ya nafaka na mizizi.

Amesema ili kukidhi mahitaji ya Wakulima hao Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeelekeza waagizaji, wazalishaji na wasambazaji wa mbolea nchini kufungasha mbolea katika ujazo unaotofautiana kuanzia kilo 5, 10, 25 na 50 ili kumwezesha kila mkulima kupata mbolea kutokana na mahitaji yake.

Waziri Bashe alikuwa alijibu swali la Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaweka utaratibu wa mbolea kuwekwa kwenye vifungashio vya kilo 5, 10, 15, 25 na 50.

Ameongeza kuwa tayari kampuni tatu zimeanza kufungasha mbolea kwa ujazo tofauti ambazo ni ETG Limited, YARA Tanzania Limited na Minjingu Mines and Fertiliser Limited.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live