Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbivu Mbichi Bajeti Kuu kujulikana kesho

Bdf20ec6d589db92d04487926fe119d9 Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Macho na masikio ya Watanzania wiki hii yataelekea bungeni, Dodoma, ambapo kesho serikali itaweka hadharani bajeti kuu yake kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Mapendekezo ya ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2022/23 uliowasilishwa Machi 11, mwaka huu na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Lameck Mwigulu yalionesha serikali imepanga kutumia Sh trilioni 41.063 ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.1 ya bajeti inayomalizika.

Bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/22 ni Sh trilioni 37.98 ikiwa ni baada ya kuwapo kwa ongezeko la matumizi ya Sh trilioni 1.3 zilizoidhinishwa na wabunge katika Mkutano wa Sita wa Bunge la 12.

Katika fedha hizo, Sh trilioni 23 zilitengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh trilioni 14.9 zilitengwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Mapendekezo ya ukomo wa bajeti kwa mwaka 2022/23 yanaonesha Sh trilioni 25.542 zimepangwa kuelekezwa kwenye matumizi ya kawaida ambayo ni asilimia 62.2 ya bajeti yote, zikijumuishwa Sh trilioni 11.38 kwa ajili ya ulipaji deni la serikali na gharama nyingine na Sh trilioni 9.740 kwa ajili ya mishahara ikijumusha mapendekezo ya upandishaji madaraja na ajira mpya, huku Sh trilioni 4.493 ni kwa ajili ya matumizi mengine.

Mapandekezo hayo yalionesha fedha zitakazoelekezwa kwenye matumizi ya miradi ya maendeleo ni Sh trilioni 15.521 sawa na aslimia 37.8 ya bajeti yote na Sh trilioni 12.122 ni fedha za ndani sawa na asilimia 78.1 ya bajeti ya Sh trilioni 3.399 ya fedha za nje.

Bajeti imelenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kijamii na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ikiwamo ya reli ya kisasa na mradi wa umeme wa Julius Nyerere.

Serikali inatarajiwa kuwa na bajeti yenye mikakati ya kuondoa mianya na kujenga mazingira ya ukusanyaji mapato.

Katika bajeti hiyo, kunatarajiwa kuwa na ongezeko na punguzo la tozo, ada na ushuru katika bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ndani na nje ya nchi kama ilivyokuwa katika bajeti zilizopita.

Maeneo mengine muhimu yanayotarajiwa kuguswa ni unafuu wa kodi kwenye sekta ya viwanda, kilimo, mifugo, madini na huduma muhimu za kijamii kwa lengo la kudhibiti mfumuko wa bei na kulinda viwanda vya ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live