Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbio Mr. UK Marathon kusomesha wajasiriamali

MARATHON ED Mbio Mr. UK Marathon kusomesha wajasiriamali

Tue, 25 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mbio hizo za kilometa tano, 10 na 21, zinatarajiwa kufanyika Julai mwaka huu kwenye viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam zikishirikisha wakimbiaji wa ndani na nje ya nchi zikiwa na lengo la kuhamasisha uwekezaji.

Mratibu wa mbio hizo ambazo zinafanyika kwa mara ya kwanza nchini, Nelson Mrashan, alisema jijini Dar es Salaam juzi kuwa, zitahamasisha uwekezaji, na kwamba ni fursa kwa wajasiriamali wadogo kufaidika kwa kupatiwa mafunzo ya muda.

"Sehemu ya mapato tutakayopata katika mbio hizo, tutawasomesha wajasiriamali wadogo kupata mafunzo zaidi SIDO ya muda mfupi na mrefu ili kuwaongezea uwezo katika shughuli zao," alisema Mrashan.

Aidha, Mrashani alisema tayari usajili kwa washiriki wa mbio hizo zenye kaulimbiu 'Mbio Kuelekea Uwekezaji', umeshaanza na kwamba zinatarajia kuwa na washiriki 2,500.

Chanzo: ippmedia.com