Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbegu ya mpunga supa yaboreshwa kukabili mabadiliko ya tabianchi

0c330f419bfd9bd6db562cd6455d4543 Mbegu ya mpunga supa yaboreshwa kukabili mabadiliko ya tabianchi

Tue, 4 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MBEGU za mpunga zinazotokana na maboresho ya mbegu za kienyeji, ikiwamo supa zimezalishwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na upungufu wa mvua.

Meneja kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Ifakara Morogoro, Dk Atugonza Bilaro alisema hayo katika viwanja vya Maonesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu Nanenane vilivyopo Nyakabindi mkoani wa Simiyu.

Alisema mbegu hizo pia zina tija kwa wakulima wale ambao wanahitaji kulima misimu zaidi ya mmoja kwa mwaka, kwani zinatoa mavuno mengi hadi mara tatu ya mbegu za kienyeji.

Dk Bilaro alitoa mfano kwa kusema mbegu aina ya TARI RIC1 imetengenezwa mahsusi kuwa mbadala wa aina ya mbegu ya supa kwa kuwa ina mavuno mara mbili zaidi.

Pia alisema aina ya TARI RIC2 imetengenezwa mahsusi kwa kilimo cha kutegemea mvua pia inakomaa mapema kiasi cha kuwezesha wakulima wenye maeneo ya umwagiiaji kulima mara mbili au zaidi kwa mwaka.

Aliongeza kuwa taasisi hiyo ya utafiti ina mbegu za mpunga zinazofaa kulimwa maeneo yasiyotuamisha maji aina ya NERICA na zile zinazovumilia kwenye maeneo ya chumvi chumvi ambazo ni SATO1 na SATO9.

“Mbegu zote hizi zinapatikana TARI Ifakara na Dakawa,” alisema. Alisema mavuno ya mbegu hizo ni wastani wa tani sita hadi nane kwa hekta tofauti na mbegu za kienyeji ambazo huzaa wastani wa tani 0.5 hadi 1.5

Chanzo: habarileo.co.tz