Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbarawa aipa CRMBEG miezi sita kukamlishaujenzi bandari Bukoba

Sekta Ya Usafirishaji Inahitaji Wataalamu Wa Kutosha   Prof Mbarawa.jpeg Mbarawa aipa CRMBEG miezi sita kukamlishaujenzi bandari Bukoba

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi Kampuni ya China Railway Major Bridge Enginnering Limited (CRMBEG) kuhakikisha mradi wa maboresho katika Bandari ya Bukoba na Kemondo unakamilika mwezi Mei mwakani ili kuruhusu meli ya MV. Mwanza kuweza kutoa huduma katika bandari hizo.

Akizungumza mara baada ya kukagua miradi hiyo mkoani Kagera Waziri Mbarawa amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutarahisisha shughuli za uchukuzi baina ya bandari hiyo, mikoa ya kanda ya Ziwa na nchi Jirani zinazunguka mikoa hiyo.

Pia ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na mradi huo kuhakikisha vifaa maalum vya kuongozea meli vinawekwa katika ziwa Viktoria ili kuziwezesha kutoa huduma katika hali ya usalama.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Kanali Wilson Sakulo ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwekeza fedha katika usafiri majini na miundombinu yake kwani kukamilika kwa miradi hiyo kutachochea ukuaji wa biashara kwa mikoa ya kanda ya Ziwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live