CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Masasi, Mtwara na Nanyumbu (MAMCU LTD) kimeuza mbaazi tani 671 zenye thamani ya Sh bilioni 1.3 kwa njia ya mnada.
Mnada huo ni wa sita na wa mwisho katika msimu wa mauzo kwa mwaka 2023/24 ulimefanyika katika Chama cha Msingi cha Chipuputa ( AMCOS) kilichopo Kijiji cha Chipuputa wilayani Nanyumbu mkoani humo.
Meneja wa MAMCU Tawi la Masasi, Costantine Leula amesema, mnada huo umefanyika leo na wameuza tani hizo 671 zenye thamani hiyo ya Sh bilioni 1.3, huku mnada wa kwanza mapaka wa sita jumla wameuza tani 11, 700 zenye thamani ya Sh bilioni 23.6.
Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu mkoani humo, Mariam Chaurembo amewapongeza wananchi wilaya hiyo kwa kuendelea kulima mazao mengine, mbadala ya korosho ikiwemo ufuta, mbaazi na mazao mengine ya chakula.
"Niwapongeze sana wananchi kwa kuona umuhimu wa mazao mengine mbadala ya kulima, niwapongeze sana mmelima sana ufuta mwaka huu, mmelima na mbaazi na mengine ya chakula hongereni sana,",amesema Chaurembo.
Katika mnada mnada huo wa sita kilo moja ya mbaazi bei ya juu ilikuwa Sh 2002 na bei ya chini ilikuwa Sh 2000. -