Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazingira wezeshi yatajwa kusaidia wawekezaji sekta ya madini

Madini Pic Data Mazingira wezeshi yatajwa kusaidia wawekezaji sekta ya madini

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya viongozi wa dini na mila wilayani Longido Mkoa wa Arusha wamefanya dua maalum, wakiishukuru Serikali kwa kuwekewa mazingira rafiki yanayowawezesha wachimbaji madini kwa faida.

Akizungumza katika dua hiyo iliyofanyika Novemba 24, kiongozi wa mila la kabila la Wamaasai wilayani humo (Laigwanan), Peter Sengeyon amesema katika kijiji hicho cha Mundarara, familia zaidi ya 100 kutoka kijijini hapo zimenufaika na ajira katika mgodi wa mwekezaji Bilionea Sendeu Laizer.

"Tunashukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji kwani sisi wa Mundarara na Longido kwa ujumla, tumeshuhudia vijana zaidi ya 100 wakijishughulisha na shughuli za uchimbaji kule mgodini kwa Laizer, hivyo familia zao zinanufaika kupitia yeye.

"Mungu ametubariki leo kupitia yeye makundi mengi ya kijamii ikiwemo watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kuchangia mradi wa maji na shule, tunaomba na wafanyabishara wengine wachangie katika shughuli za kijamii, hii tumeweza kufanya kutokana na amani ambayo tuko nayo katika nchi yetu," amesema Sengeyon.

Kwa upande wake Bilionea Laizer amesema mazingira rafiki na amani iliyopo nchini inawezesha wachimbaji kufanya shughuli zao kwa uhuru na wananchi wamekuwa wakinufaishwa na miradi ukiwemo ya ujenzi wa shule, maji na elimu kwa watoto wanaotoka katika familia duni na yatima inayotekelezwa na mwekezaji huyo.

"Sisi wawekezaji katika wilaya hii na nchini kwa ujumla tunafanya shughuli zetu bila kuwa na usumbufu wa aina yoyote kutokana na mazingira haya rafiki tuliyowekewa na Serikali kuvutia wawekezaji," amesema Laizer.

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Longido, Papa Nakuta amesema Serikali imepeleka miradiya maendeleo ya zaidi ya Sh14 bilioni kwa ajili ya mkoani Arusha, huku akimpongeza mwekezaji huyo kwa uhusiano mzuri baina yake na jamii inayomzunguka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live