Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawaziri wajifungia kujadili sekta ya uvuvi

Meli  Uvuviii.png Mawaziri wajifungia kujadili sekta ya uvuvi

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amekutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo na kufanya mazungumzo yaliyolenga kufahamu vipaumbele muhimu vya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambavyo vitajumuishwa katika mapendekezo yatakayosaidia kuandaliwa kwa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka 2024/2025.

Katika kikao hicho ambacho kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi, jijini Dodoma, Prof. Kitila aliongeza kuwa, kikao hicho kimelenga kuleta ushirikishwaji wa sekta katika maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2024/2025.

Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameahidi kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ili sekta za mifugo na uvuvi ziweze kutekeleza majukumu yake sambamba na Mpango wa Maendeleo wa Taifa.

Aidha, Ulega ameomba masuala yanayohusu uanzishwaji wa Mamlaka inayosimamia Uvuvi, Chanjo ya Mifugo , Bandari ya Uvuvi ya Bagamoyo na Uchumi wa buluu na Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT-LIFE) kujumuishwa katika mapendekezo hayo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida ametoa rai kwa Wizara hiyo kuzingatia uzalishaji wenye tija na upatikanaji wa masoko wa bidhaa zinazozalishwa huku akigusia matumizi ya teknolojia katika uzalishaji akitolea mfano ufugaji wa Samaki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live