Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kanda ya kati iimewafikisha mahakamani mawakala wa mbolea 14 katika mikoa mitatu ya kanda ya kati kwa kufanya ubadhirifu kwenye biashara hiyo. Kwa mujibu wa TFRA, mawakala wawili ni wa mkoa wa Dodoma, Tabora watano na Kigoma saba. Hayo yamesemwa Ijumaa Agosti 4, 2023 na Kaimu Meneja wa TFRA kanda ya kati, Joshua Ng’ondya wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la mamlaka hayo katika uwanja wa nanenane Nzuguni jijini Dodoma. “Kuna wengine katika mpango wa ruzuku wamenunua namba za wakulima, wapo waliochakachua mbolea kwa mfano tulisema usipime lakini wao wanafungua mfuko na kupima lakini wengine wanauza juu ya bei elekezi,”amesema. Amesema mawakala hao walipigwa faini,kufikishwa mahakami na wengine walifutiwa leseni zao za uwakala wa mbolea. Ngo’ndya amechasambaza madaftari ya usajili ili wakulima waweze kupata namba ambazo zitawawezesha kununua mbolea kwenye msimu huu wa kilimo. Amesema kwa wakulima waliojisajili msimu uliopita wamepeleka madaftari kwa ajili ya uhakiki ili wale waliokuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuongeza eneo la kilimo waweze kuhuisha taarifa zao. Amesema ili kuondoa changamoto za upatikanaji wa mbolea karibu na mashamba sasa wakulima wataweza kupata mbolea kupitia vyama vya ushirika. “Sasa tumetumia vyama vya ushirika ili kuondoa changamoto za msimu uliopita, mamlaka inataka kuhakikisha mkulima hatembeli zaidi ya kilometa 15 kufuata mbolea,”amesema. Amesema mawakala 158 wamepata mafunzo kuhusu mfumo mpya utakaoanza kufanya kazi katika msimu wa kilimo ujao ambao utakwenda kutatua changamoto za mtandao. Ng’ondya amesema katika msimu uliopita mwitikio wa usajili ulikuwa chini kutokana na matumizi ya chini ya mbolea baada ya wengi kuamini kuwa mbolea zinaharibu dongo. “Lakini kupitia maonyesho ya nanenane na kupitia watalaam wetu tumewaelimisha kuwa mbolea haiharibu udongo. Tunasisitiza matumizi sahihi ya mbolea, tumewaelimisha namna ya kutumia mbolea, changamoto hii imekwisha na sasa wanaendelea kupata mbolea,”amesema. Naye mmoja wa wakulima waliotembelea banda hilo, Rhoda Maheneko amesema elimu aliyoipata kupitia maonyesho hayo imemsaidia kuhusu uelewa wa umuhimu wa mbolea katika kilimo anachokifanya. “Tuliaminishwa kuwa mbolea ni mbaya katika kilimo lakini kwa elimu niliyoipata sasa nitajisajili nianze kutumia mbolea kwenye shamba langu la alizeti,”amesema Rhoda.