Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde kutoa Sh20 milioni kwa wajasiriamali

Fedhapic Mavunde kutoa Sh20 milioni kwa wajasiriamali

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde ameanzisha tuzo maalum ya wajasiriamali ambayo italenga katika kuongeza wigo wa uchakataji bidhaa za kilimo na mifugo kwa kukipatia mitambo na mashine ndogo zenye thamani ya Sh20 milioni kwa kikundi kimoja kitakachopitishwa na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) kila mwaka.

Mavunde ameyasema hayo jana Mei 30, 2023 katika Viwanja vya Nyerere Square wakati akifunga mafunzo ya wajasiriamali mkoani Dodoma chini ya mwavuli wa Taasisi ya Wanawake na Uchumi wa Viwanda (WAUVI).

“Ninawapongeza sana WAUVI kwa mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo wajasiriamali wa Dodoma ili kuongeza thamani ya bidhaa wanazozalisha.

Nitaanzisha tuzo ya Mavunde ya Wajasiriamali ambayo lengo lake kubwa litakuwa ni kupata kikundi cha kuongeza thamani ya mazao na mifugo ambacho tutakipa mitambo na mashine ya Sh20 milioni na kukilea mpaka kukua kwake,” alisema Mavunde.

Mavunde amevutiwa na jitihada za wajasiriamali hao wa mkoa wa Dodoma huku akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutengeneza fursa nyingi zaidi za kiuchumi kupitia uwekezaji mkubwa unaoendelea wa kuijenga makao makuu Dodoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live