Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde awaita wawekezaji nchini

Antony Mavunde.jpeg Mavunde awaita wawekezaji nchini

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde amewakaribisha wawekezaji wa viwanda vya uzalishaji wa betri za magari ya umeme na vifaa vya kieletroniki kuwekeza nchini.

Mavunde amesema Tanzania imebarikiwa madini mkakati ya kutosha ambayo ni malighafi kuu ya uzalishaji wa betri za magari ya umeme na vifaa vya kieletroniki.

Ameyasema hayo Kwamsisi, wilayani Handeni mkoani Tanga wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji madini mkakati ya kinywe (Graphite) kinachomilikiwa na Kampuni ya Godmwanga Germs Ltd.

“Uwekezaji huu unatokana na mazingira mazuri na wezeshi yaliyowekwa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, " amesema Mavunde.

Aidha, amempongeza Mwekezaji Mtanzania God Mwanga kwa kuwa mmoja kati ya wawekezaji wakubwa wa madini nchini Tanzania na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta ya madini na upatikanaji wa nafasi za ajira kwa watanzania.

"Mkakati wa serikali ni kuhakikisha madini haya yanaongezwa thamani nchini Tanzania ili kutunza ajira za watanzania,kuwajengea uwezo na kukuza uchumi wa taifa kupitia kodi na mapato mbalimbali.

"Hivyo niwakaribishe wawekezaji wote wenye nia ya kuongeza thamani mkakati haya kuitumia fursa hii kwa kuwa Tanzania imebarikiwa madini mengi na ya kila aina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live