Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde awafungulia 'code' wafanyabiashara wa madini

Biteko Madini Mavunde awafungulia 'code' wafanyabiashara wa madini

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde ameshauriwa na wamiliki wa migodi ya madini ya Tanzanite kuwa macho dhidi ya wataalamu waangalizi wa serikali maarufu ’jicho la serikali’.

Imeripotiwa kutoka kwa wamiliki hao kuwa wataalam hao wako kwa ajili ya kujinufaisha na kufanya serikali kupoteza mamilioni ya fedha za kodi katika tathmini ya madini hayo.

Mmoja wa wamiliki wa mgodi wa madini ya Tanzanite ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake amesema pamoja na kupeleka malalamiko kwa Ofisa Madini Mfawidhi Mirerani, Nchahwa Chacha bila majibu wameamua kumwandikia barua Waziri Mvunde juu ya hali hiyo.

Mmiliki huyo amesema waangalizi hao wa serikali mara baada ya mgodi kutoa uzalishaji wa madini ya Tanzanite huja katika mgodi na kuanza kupora madini, kuyaficha na kwenda kwenye tathmni ambapo madini machache na yasiyokuwa na thamani na serikali ndio yanabaki na hivyo kukosa mapato kwani madini mazuri yamechukuliwa na watalaamu hao

Chanzo: www.tanzaniaweb.live