Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde atoa mwelekeo mpya sekta ya madini

Mavunde Atoa Mwelekeo Mpya Sekta Ya Madini Mavunde atoa mwelekeo mpya sekta ya madini

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mikakati ya kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa shughuli za utafiti wa madini nchini kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili kutoa taarifa sahihi za kijiolojia za madini na kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi sambamba na kuwawezesha wachimbaji wadogo.

Waziri wa Madini, Mhe Anthony Mavunde (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 11 Septemba 2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye kikao cha pamoja kati ya wachimbaji wadogo chini ya mwamvuli wa FEMATA.

Amesema kuwa, ili kuongeza uwekezaji katika Sekta ya Madini, Wizara kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeweka mkakati wa kuhakikisha tafiti za kijiolojia zinafanyika katika maeneo yote nchini ifikapo mwaka 2030 ili kuwezesha wachimbaji wa madini wengi kuendesha shughuli zao bila kubahatisha na Serikali kuendelea kupata mapato ambayo yatawezesha kuimarisha sekta nyingine muhimu kama vile miundombinu, kilimo, nishati n.k.

“Tafiti hizi zitawezesha kugundulika kwa madini ya kimkakati, malighafi kwa ajili ya kuzalisha mbolea hali itakayopelekea uwepo wa viwanda vya kuzalisha mbolea nchini, kuzalisha ajira mpya katika Sekta ya Madini na sekta nyingine na kupunguza migogoro kati ya wachimbaji wadogo wa madini na wachimbaji wakubwa wa madini,” amesema Mavunde.

Katika hatua nyingine, amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko alipokuwa Waziri wa Madini na kuongeza kuwa ataendeleza kazi nzuri iliyofanywa sambamba na kuomba ushirikiano kwa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini ili kuhakikisha mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa unafikiwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025 huku wananchi wakiendelea kutajirika kutokana na uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Aidha, amepongeza kasi ya Tume ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini hasa kwenye ongezeko la ukusanyaji wa maduhuli kila mwaka, uanzishwaji wa masoko ya madini 42 na vituo vya ununuzi wa madini nchini 95, kuimarika kwa usimamizi wa usalama wa afya na mazingira kwenye shughuli za uchimbaji wa madini na kuitaka Tume kuongeza ubunifu kwenye utendaji kazi.

Waziri Mavunde amesema kuwa hatoangalia sura ya mtu wala Cheo Kwenye Utoroshaji wa Madini badala yake atakula sahani moja na kila mbadhilifu anayetorosha madini kwani ni kinyume na taratibu sambamba na sheria ya madini.

Naye Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa akizungumza kwenye kikao hicho sambamba na kupongeza kwa uteuzi wa Waziri Mavunde amesema kuwa Wizara na Taasisi zake ipo tayari kumpa ushirikiano ili kuhakikisha Sekta ya Madini inakuwa miongoni mwa sekta zinazoongoza mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live