Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde ataka haya sekta ya madini

Madini Pic Data Mavunde ataka haya sekta ya madini

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), imeiwezesha sekta ya madini kupiga hatua kiuchumi ikiwemo kuchangia asilimia 56 ya thamani ya bidhaa za madini zilizouzwa nje katika Mwaka wa Fedha 2022/23.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Anthony Mavunde jijini Dar es Salaam katika kikao cha wadau wa madini, zikiwemo taasisi za umma na binafsi zinazojishughulisha na Sekta ya Fedha chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA).

Amesema, sekta ya madini imechangia kodi za ndani kwa asilimia 15 ambazo ni sawa na Sh trilioni 2 pamoja na kuchangia Dola za Marekani Bilioni 3.3. kutokana na mauzo ya bidhaa zinazotokana na rasilimali madini.

Mavunde amesema, wizara itawezesha kufanyika kwa utafiti wa angalau kufikia asilimia 50 ifikiapo mwaka 2030 kwa ushirikiano wa taasisi hizo, tafiti hizo zitaliwezesha taifa kupiga hatua kubwa zaidi za kimaendeleo na kiuchumi kupitia sekta ya madini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live