Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde ashusha rungu utoroshaji madini

MAVUNDEEEEEE Mavunde ashusha rungu utoroshaji madini

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imesimamisha leseni zote nchi nzima za Kampuni ya Nadoyoo Mineral Trading kufuatia kukamatwa kwa mmoja wa wahusika wa kampuni hiyo akituhumiwa kutorosha dhahabu zaidi ya kilo 4.3 zenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 562.3. -

Dhahabu hizo zimekamatwa katika operesheni ya kushtukiza iliyofanywa usiku na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. -

Akizungumza mara baada ya dhahabu hiyo kukamatwa, Mavunde amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, haitakubali kuona watu wachache wanajihusisha na vitendo hivyo viovu vya kutorosha madini. -

"Nataka niwaambie, tutachukua hatua kali dhidi ya yeyote tutakayemkamata akijihusisha na utoroshaji wa madini, "amesema Mavunde na kuongeza: -

"Nilipoingia Wizara ya Madini mwezi mmoja uliopita nilisema, ukitaka kufahamu sura yangu nyingine basi jaribu kutorosha madini.;.... Sasa basi, kuanzia leo mtu yeyote atayekamatwa kwa kosa la kutorosha madini, tutakwenda kusimamisha leseni zake zote nchi nzima wakati tukisubiri hukumu ya vyombo vya sheria," amesema. -

Amesema, iwapo mahakama itabaini mhusika ana hatia, atachukuliwa hatua kali ikiwem -

Mavunde ametoa wito kwa wafanyabiashara wa madini kuwa wazalendo kwa kufuata taratibu zilizopo na kulipa tozo, ada na kodi mbalimbali ili kuiwezesha serikali kupata mapato na kuendelea kuimarisha huduma kwa wananchi ikiwemo ujenzi wa barabara, umeme, afya na elimu. -

Amesema, yupo tayari kukaa na wafanyabiashara wa madini ili kwa pamoja wamweleze hasa ni nini wanadhani inaweza kuwa ni changamoto kubwa inayopelekea baadhi yao kufikia hatua ya kujihusisha na vitendo vya utoroshaji madini, hatua ambayo anaamini itasaidia Serikali kuchukua njia sahihi kushughulikia suala hilo. - Vilevile, ameweka bayana kuwa pamoja na hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya watoroshaji wa madini, pia madini yote yatakayokamatwa yatahifadhiwa na serikali na kupelekwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kusubiri hatma ya Mahakama. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live