Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde akoshwa na GF TRUCK

MAVUNDEEEEEE Mavunde akoshwa na GF TRUCK

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameipongeza kampuni ya GF TRUCK kwa kufungua ofisi mkoani Geita na kuona umuhimu wa kushirikiana na sekta ya madini hasa wachimbaji kuwapatia vifaa.

Kampuni hiyo leo Septemba 25,2023 imezindua ofisi iliyopo katika soko kuu la dhahabu Geita na kukabidhi maroli matatu yaliyonunuliwa na wachimbaji.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mavunde amesema itarahisisha shughuli za uchimbaji ili Watanzania washiriki kikamilifu katika sekta ya madini.

“Nawapongeza kwa kuamua kusogeza huduma karibu kabisa na wachimbaji, niwaombe muendelee kutanua wigo, wachimbaji ni waaminifu wanao uwezo mkubwa wa kuchukua mitambo kwa njia ya mkopo na kuirejesha,” amesema Mavunde.

Amesema pia mwaka huu Mkoa wa Geita umewekewa lengo la kukusanya maduhuli ya Serikali Sh243 bilioni na ndio mkoa unaoongoza kwa mchango mkubwa wa maduhuli.

Mkurugenzi wa masoko na biashara wa kampuni ya GF TRUCK, Salman Karmali amesema walianza kufanya upanuzi wa kiwanda kwa lengo la kuanza kuunganisha magari madogo na mwaka huu wanatarajia kuunganisha magari 1,500.

Amesema waliingia makubaliano na Shirika la Madini la Taifa (Stamico) ambalo lina vifaa vya kuchoronga na kufanya tafiti huku kampuni hiyo ikitoa mashine na maroli.

Aidha, amesema wamekubaliana kuweka mashine karibu na wachimbaji ili kuwa karibu na wachimbaji wadogo.

“Geita inategemea uchimbaji kwa asilimia kubwa na sisi GF TRUCK tunategemea wana Geita, magari tunayouza ni matunda mazuri ya Serikali. Tunajivunia kiwanda chetu kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani ambacho ni kiwanda pekee cha kuunganisha magari,” amesema Karmali

Chanzo: www.tanzaniaweb.live