Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde aamkia kituo cha jiolojia

MAVUNDEEEEEE Mavunde amkia kituo cha jiolojia

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameahidi kuipa ushirikiano Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini katika kutekeleza majukumu yake ili kuongeza mchango wa sekta ya madini lakini pia kuiwezesha Taasisi ya Utafiti wa Jiolojia nchini (GST) ili ilete tija.

Ameyasema hayo jana Septemba 5, 2023 alipokutana na Kamati hiyo jijini Dodoma ili kuzungumzia mwenendo wa biashara na shughuli za sekta ya madini sambamba na kufahamiana na Kamati baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Madini.

"Ninawaahidi kuwapa ushirikiano katika kipindi chote ninyi kama Kamati ya Bunge ili kwa pamoja tushirikiane katika mageuzi haya kwenye sekta hii muhimu hapa nchini," amesema Mhe. Mavunde.

Pia, Mavunde ameieleza Kamati hiyo kuwa Wizara imeandaa mpango wa kuiwezesha Taasisi ya Utafiti wa Jiolojia Tanzania (GST) kwa kuipatia vifaa na teknolojia ya kisasa zaidi ili ifanye utafiti wa kutosha kuendana na mahitaji ya sasa ya Dunia na kuibua maeneo mengi zaidi yaliyo na madini hapa nchini ili kuongeza wigo wa Sekta hiyo sambamba na mchango wake katika Pato la Taifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ussi Pondeza amesisitiza kuwa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini itatoa ushirikiano kwa Waziri Mavunde na timu yake ili Sekta ya Madini iwanufaishe Watanzania kupitia uchumi wa madini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live