Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde: Tutafuta leseni za watakaotorosha madini

MAVUNDEEEEEE Mavunde: Tutafuta leseni za watakaotorosha madini

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema hatamuonea aibu mtu yeyote atakayejihusisha na utoroshwaji wa Madini na ikibidi atafuta leseni yake.

Akifungua mkutano wa majadiliano kuhusu mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa sekta ya madini nchini unaofanyika mkoani Dar Mavunde amesema, atafuta leseni na kumuweka katika orodha isiyofaa mchimbaji yeyote atakayebainika kutorosha madini.

Waziri Mavunde amesema kama Kuna changamoto ambayo inasababisha utoroshwaji wa Madini basi izungumzwe na kupatiwa ufumbuzi badala ya kuhujumu uchumi.

Ameongeza kuwa, Madini ndio sekta kiongozi hivyo kila mdau anapaswa kuhakikisha maono ya Serikali katika sekta hiyo yanafikiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live