Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde: GST ndio moyo sekta ya madini

Madini Pic Data Mavunde: GST ndio moyo sekta ya madini

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema Taasisi ya Jiolojia na Ufafiti wa Madini Tanzania (GST) ndiyo moyo wa Sekta ya Madini na ni Taasisi inayotegemewa na Wizara ya Madini na Sekta ambata kama Sekta ya Maji, Kilimo na Ujenzi. - Mavunde ameyasema hayo baada ya kukutana na kuzungumza na watumishi wa GST Septemba 04, 2023, jijini Dodoma. - "Kulingana na historia GST ni kinara wa utoaji wa taarifa za masuala ya Jiolojia Barani Afrika hivyo hakikisheni mnaweka mikakati ya kufanya Taasisi hii iwe Bora zaidi katika sekta ya madini" amesema Mavunde. - "Dunia kwa sasa inahitaji Madini ya Kimkakati ikiwemo Kinywe, Lithium na Nikeli kwa ajili ya mahitaji ya tecknolojia ya kisasa na ifikapo mwaka 2050 inategemewa kuwa mahitaji ya madini hayo yatakuwa mara miatatu zaidi ya yalivyo kwasasa," amesema Mavunde. - Aidha, Mavunde ameitaka GST kutengeneze mashirikiano na taasisi zingine za utafiti wa Madini duniani kwa lengo la kupata uzoefu, ujuzi na uwezo wa taasisi wa kupata vifaa vya kisasa zaidi na kuwa na Maabara Bora Barani Afrika na kuifanya taasisi hiyo kuwa sehemu ya utambulisho wa Tanzania. - Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya GST, Prof. Idris Ikingula amesema jukumu kubwa la GST ni kufanya utafiti wa jiosayansi kwa lengo la kubaini rasilimali zilizopo ardhini ikiwa ni pamoja na aina za miamba sambamba na madini yanayopatikana kwenye miamba hiyo katika maeneo mbalimbali ya nchini. - Naye, Mtendaji Mkuu wa GST, Dk. Mussa Budeba amewasilisha mada ya mwenendo mzima wa shughuli za Utafiti ambapo amesema lengo la tafiti zinazofanywa na GST ni kuibua maeneo mapya yenye madini na hatimaye kuanzishwa kwa migodi mipya au uchimbaji wa madini. - Tafiti za jiosayansi ambazo zimefanywa na GST ndizo chanzo cha kuanzishwa kwa migodi mbalimbali nchini kwa kutumia taarifa zake ikiwemo Geita Gold Mine (GGM), Bulyanhulu Gold Mine, Twiga Gold Mine, Nyanzaga Gold Mine, Shanta Gold Mine - Singida, Migodi ya Makaa ya Mawe na sehemu nyingine zenye uchimbaji mdogo na wa kati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live