Menu ›
Biashara
Fri, 3 May 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema uzalishaji wa zao la parachichi umeongezeka na kufikia tani 26,826.30 mwaka 2022/2023 kutoka tano 17,711.49 mwaka 2021/2022.
Kufuatia ongezeko hilo pia mauzo ya zao hilo yamepanda hadi kufikia dola Milioni 77.3 za Kimarekani mwaka 2022/2023 kutoka dola Milioni 51 mwaka 2021/2022.
Waziri Bashe alikuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 bungeni jijini Dodoma.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live