Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maumivu pande zote, nauli za meli nazo zapanda

Meli Pic Data Maumivu pande zote, nauli za meli nazo zapanda

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) imetaja sababu ya kupanda kwa nauli za meli zake ni kupanda kwa gharama za uendeshaji kunakosababishwa na ongezeko la bei ya mafuta.

 Gharama za nauli ya kusafirisha abiria na mizigo kwa njia ya maji kati ya miji ya Mwanza na Bukoba kwa meli ya Mv Victoria "Hapa Kazi Tu" na Mv Butiama inayotoa huduma kati ya Mwanza na Ukerewe imepanda kwa wastani wa Sh2, 445 hadi Sh10, 000 kwa safari.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa Julai 1, 2022 na Idara ya Masoko na Mauzo ya MSCL ilionyesha kwamba nauli ya daraja la uchumi iliyokuwa Sh16,000 kwa mtu mzima imepanda hadi Sh21,000 huku nauli ya mtoto ikipanda kutoka Sh8, 550 hadi Sh11,000.

Akizungumza jana Jumanne Julai 5, 2022 ofisini kwake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa MSCL, Philemon Bagambilana amesema nauli mpya katika meli hizo zilianza kutumika Julai 4,2022 huku akiwatoa hofu abiria kwamba upandaji wa nauli hizo umezingatia sheria na taratibu za upandishaji wa nauli nchini.

Amesema pamoja na mabadiliko katika gharama za uendeshaji na ongezeko kwenye bei ya mafuta duniani, kampuni hiyo haijawahi kufanya maboresho ya nauli katika meli zake jambo linalosababisha ugumu katika uendeshaji wa meli hizo.

"Hatujipandishii tu kwa matakwa yetu tunafuata miongozo na tunadhibitiwa na mamlaka (Shirika la wakala wa meli Tanzania -TASAC) tusipofanya hivyo basi huduma hizi hazitakuwepo, kwahiyo hatujatoka nje ya utaratibu na hatujataka kuwaumiza abiria kwani dhana ya kuwahudumia wananchi iko pale pale," amesema Bagambila.

Advertisement Kwa upande wake, Meneja Masoko na Mauzo wa MSCL, Anselm Namala amesema ongezeko la nauli hizo halijaathiri uwepo wa wateja katika meli hizo huku akiahidi kuendelea kuboresha huduma ili ziendane na mabadiliko hayo.

"Hatujapandisha tu nauli bali tumeboresha pia huduma zetu ambapo wateja watapata vinywaji tunataka mabadiliko haya yaende sambamba na maboresho ya huduma ili tuipe thamani fedha ya mteja.”

“Tutaendelea kuwazingatia wananchi na kujali haki zao na tunawaomba waendelee kulinda usafiri huu dhidi ya uharibifu," amesema Namala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live