Shirika la Chakula Duniani, FAO, limesema bei za vyakula duniani zilipungua mwezi Desemba na kuashiria kushuka kwa mwezi wa tisa mfululizo, ingawa zilifikia kiwango cha juu zaidi katika rekodi ya mwaka mzima wa 2022.
Faharasa ya bei ya chakula ya FAO, ambayo inafuatilia bei za chakula kimataifa, imeshuka hadi wastani wa alama 132.4 mwezi uliopita ikilinganishwa na alama 135.00 iliyofanyiwa marekebisho mwezi Novemba.
Aidha, FAO, bei ya vyakula ilipanda hadi rekodi ya juu mwezi Machi baada ya Urusi kuivamia Ukraine, ambayo ni msambazaji mkubwa wa ngano na mafuta ya kupikia duniani.
Kushuka kwa bei mwezi Desemba kumesababishwa na kupungua kwa bei ya kimataifa ya mafuta ya kupikia pamoja na nafaka na nyama. Ingawa rekodi ya bei ya chakula iliongezeka kutokana na kuongezeka kwa bei ya sukari na maziwa.