Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matunda ya uwekezaji: Bandari yakusanya Bil. 5 Januari-Machi

Matunda Ya Uwekezaji: Bandari Yakusanya Bil. 5 Januari Machi Matunda ya uwekezaji: Bandari yakusanya Bil. 5 Januari-Machi

Mon, 3 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matunda ya uwekezaji katika Bandari ya Tanga yameanza kuonekana baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete kueleza kwamba bandari hiyo imefanikiwa kukusanya mapato ya Sh.Bilioni 5 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu

Mwakibete aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja kutembelea Bandari hiyo ambapo alisema kwamba mapato hayo yametokana na kukamilika kwa Gati hatua ambayo imesaidia kuongezeka Kwa shehena ya meli za mizigo.

Alisema kwamba hayo ndio mafanikio yaliyotokana na uwekezaji wa Takribani na Sh.Bilioni 429 uliofanywa na Serikali katika Bandari ya Tanga ambao umewezesha kuongezeka kwa shehena ya mizigo hatua ambayo imepeleka kuongezeka kiasi cha mapato hayo.

“Hii ni kazi nzuri ya uwekezaji ambao umefanywa na Serikali hatua ambayo imeleta manufaa makubwa katika Bandari ya Tanga hivyo nitoe wito kwa wafanyabiashara kuitumia Bandari ya Tanga kutokana na kuwa na uweke

Katika hatua nyengine,Naibu Waziri huyo alitoa muda wa mwezi mmoja kwa shirika la Reli Tanzani (TRC) kuhakikisha wanajenga miundombinu ya reli katika bandari ya Tanga ili kurahisha huduma za usafirishaji wa mizigo inayoshushwa kwenye bandari hiyo kuelekea maeneo mbali mbali ya nchi.

Awali akizungumza Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi alisema ndani ya kipindi Cha miezi mitatu wamepokea Meli kubwa tano ambazo zimebeba zaidi ya shehena ya mizigo Tani 130,000 .

Hata hivyo alisema kutokana na uingiaji wa Meli kubwa umesaidia kuwezesha ajira za muda mfupi 100 zimeweza kupatikana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live