Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matumizi ya Serikali kuongezeka katika bajeti ijayo

83020 Mpango+pic Matumizi ya Serikali kuongezeka katika bajeti ijayo

Fri, 8 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Matumizi ya Serikali yanakadiriwa kuongezeka kutoka Sh33.105 trilioni ya mwaka wa fedha 2019/2020 hadi Sh34.360 trilioni kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 bungeni leo Jumanne Novemba 5, 2019.

Amesema matumizi ya kawaida yanakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 4.7 hadi Sh21.66 trilioni sawa na asilimia 13.7 ya Pato la Taifa na matumizi ya maendeleo yanakadiriwa kuwa Sh12.699 trilioni sawa na asilimia 8.0 ya Pato la Taifa.

Dk Mpango amesema katika mwaka 2020/21 jumla ya misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo inatarajiwa kufikia Sh1.269 trilioni ambapo misaada ya kibajeti (General Budget Support- GBS) inatarajiwa kuwa Sh154.2 bilioni.

Amesema misaada ya mifuko ya pamoja ya kisekta (Basket Funds) Sh172.9 bilioni na misaada ya miradi (Project Funds) Sh941.5 bilioni.

Aidha, amesema nakisi ya bajeti inayojumuisha misaada inakadiriwa kuwa Sh3.943 trilioni sawa na asilimia 2.5 ya Pato la Taifa kwa mwaka 2020/21 ambapo Sh2.355 trilioni zitagharamiwa na mikopo ya nje na Sh1.588 trilioni zitagharamiwa na mikopo ya ndani sawa na asilimia 1 ya Pato la Taifa.

Chanzo: mwananchi.co.tz