Matumizi ya bidhaa zitokanazo na mbao zilizochakatwa, yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 37 ifikapo mwaka 2050, iwapo rasilimali hiyo itaendelea kutumiwa bila kuzingatia kanuni.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO, kuhusu mwelekeo wa misiti duniani mwaka 2050, imesema tathmini ya mahitaij ya siku za usoni na vyanzo mbao kwa uchumi endelevu inasema matumizi ya bidhaa za mbao yanatarajiwa kufikia mita za ujazo bilioni 3.1 ifikapo mwaka 2050.
Ripoti hiyo imesema, ongezeko la matumizi litakuwa angalau asilimia 8 zaidi pindi mazingira aina mbili yanapozingatiwa: mbao zinazokandamizwa na zile zinazotengenezwa kwa kutumia nyuzinyuzi, hizi zikichukua nafasi ya mbao zisizotumia malighafi zisizo rejelezi.
FAO imeongeza kuwa, iwapo juhudi zitawekwa katika kutumia mbao kwa teknolojia hizo mbili ongezeko la matumizi ya bidhaa za mbao linaweza kufikia asilimia 23 zaidi kuliko katika mazingira ya matumizi kwa kawaida.
Ongezeko la mahitaji ikilinganishwa na makadirio ya ongezeko la asilimia 25 la asilimia watu duniani, “litachochewa na vipato vya juu katika nchi zilizoko maeneo yanayoibuka kiuchumi watu wakihitaji makaratasi, vifungashio, nguo na samani, halikadhalika katika sekta ya ujenzi.”
Mbao ni zao rafiki kwa mazingira na inazidi kuongezeka kutumika kuchukua nafasi ya bidhaa ambazo si rafiki kwa mazingira likiwa ni muhimu katika kushughulikia tishio la madhara ya tabianchi duniani, athari zinazotishia bayonuai, vitisho visababishwavyo na matumizi ya kupitiliza ya bidhaa zisizorejeleka.