Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matumizi ETS yanavyoendelea kufanikiwa Tanzania

Matumizi ETS yanavyoendelea kufanikiwa Tanzania

Thu, 14 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Uamuzi wa Serikali kuachana na stempu za kodi za karatasi na kugeukia za kielektroniki (ETS), umeonyesha la makusanyo ya tozo na kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa bidhaa mbalimbali.

Takwimu zilizothibitishwa na kamishna wa kodi za ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Abdul Mapembe zinaonyesha makusanyo ya tozo na VAT katika mvinyo na pombe zinazozalishwa ndani yameongezeka kwa asilimia 35.3 katika robo ya kwanza ya mwaka 2019/20 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Awali, Serikali ilitangaza uamuzi wa kuanza kutumia stempu za kielektroniki Juni, 2018 huku kampuni kutoka Uswisi ya Société Industrielle et Commerciale de Produits Alimentaires (SICPA) ikishinda zabuni na kusaini mkataba na TRA ili kuweka mifumo ya usimamizi wa kodi.

Awamu ya kwanza ya ETS ilifanyika Januari 15 mwaka huu kwa kufunga mifumo ya stempu kwenye kampuni 19 zinazalisha pombe, mvinyo na pombe kali.

Awamu ya pili iliyowekwa kwenye vinywaji laini na maji ya chupa, ilianza Agosti Mosi mwaka huu.

Mfumo wa ETS unaiwezesha Serikali kutumia teknolojia ya kisasa kupata takwimu za uzalishaji kwa wakati kutoka kwa wazalishaji.

Pia, inaiwezesha Serikali kuzuia upotevu wa mapato na kutambua kiwango cha kodi kinachotakiwa kulipwa kama tozo, VAT au kodi ya mapato.

Kwa mujibu wa Mapembe, TRA ilikusanya Sh25.8 bilioni kutoka kwenye pombe na mvinyo unaozalishwa ndani ya nchi katika robo ya kwanza ya mwaka 2018/19 lakini makusanyo yaliongezeka wakati wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/20.

Tozo na VAT kwenye sigara iliongezeka kwa asilimia 5.6 katika robo ya kwanza ya mwaka 2019/20 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2018/19.

Katika sigara ilikusanya Sh56.7 bilioni kama tozo na VAT kwa Julai mpaka Septemba 2019, kutoka Sh53.7 bilioni zilizokusanywa mwaka jana.

Kwa vinywaji laini, TRA ilikusanya Sh16.155 bilioni kama tozo na VAT kutoka Agosti na Septemba 2018 lakini kiwango kiliongezeka hadi kufikia Sh19.05 bilioni kati ya Agosti na Septemba mwaka huu.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Richard Kayombo alisema matumizi ya ETS yalianzishwa ili kuchukua nafasi ya stempu za karatasi zilizokuwa zinahusishwa na ukwepaji wa kodi na utengenezaji wa bidhaa feki.

Chanzo: mwananchi.co.tz