Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masoko 54 kufunguka Afrika mkataba huu utapitishwa na Bunge la Tanzania

Mkumbo.jpeg Mkataba wa biashara kimataifa kufungua masoko 54 Afrika.

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Wizara ya Viwanda na Biashara imeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano kuridhia mkataba wa biashara huru wa Afrika ili kuiwezesha Tanzania kushindana katika biashara za kimataifa.

Hayo yamesemwa leo Agosti 13 na Waziri wa viwanda na biashara, Profesa Kitila Mkumbo alipofanya ziara katika kiwanda cha A to Z akiwa ameongozana na kamati ya Bunge ya Bajeti inayoendelea na ziara yake mkoani Arusha.

"Wizara ina mpango wa kuomba Bunge liridhie Tanzania kujiunga na mkataba wa biashara huru wa Afrika, kwani viwanda vinahitaji ushindani mkubwa Afrika na Dunia kwa ujumla na kwa kufanya hiyo tutaweza kupanua wigo mkubwa katika kufanya biashara zetu na kwa viwango vikubwa zaidi," amesema Profesa Mkumbo.

Profesa Mkumbo amesema, endapo Tanzania itasaini mkataba huo itasaidia kufungua masoko katika nchi 54 za Afrika.

Kuhusu kodi, amelitaka Bunge kujenga hoja za kuishauri Wizara ya Fedha na Mipango kuweka viwango vitakavytochochea uzalishaji katika viwanda pamoja na kuweza kushindana katika soko la ndani ya nchi na ukanda wa Afrika.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa kiwanda cha A to Z, Sylvester Kazi amesema changamoto kubwa zaidi inawayokabili ni marejesho ya VAT yanayochelewa, akiomba Kamati ya Bunge ya Bajeti isaidie ili marejesho hayo yarudi kwa wakati.

Ametaja changamoto nyingine kuwa ni ongezeko la kodi kwenye nyuzi za pamba kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 25, akiomba serikali kurudisha kwenye kiwango cha awali kwani kuna mikataba ya mauzo ambayo walishaingia na haiwezekani kuongeza bei ya bidhaa hizo tena.

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya bajeti, Daniel Baran amesema wamesikia changamoto hizo na watashirikiana na serikali kuutafuta ufumbuzi, kwani kiwanda hicho ni hulipa kodi ya zaidi ya bilioni 17 kwa mwaka.

Amesema pamoja na ulipaji wa kodi pia kiwanda kimeajiri zaidi ya Watanzania 800.

Chanzo: Mwananchi