Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashirika ya mazingira yawasilisha kesi dhidi ya TotalEnergies

Total Energies.png Mashirika ya mazingira yawasilisha kesi dhidi ya TotalEnergies

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashirika manne ya ulinzi wa mazingira yamefungua kesi dhidi ya kampuni ya mafuta ya Ufaransa, TotalEnergies, yakidai inachangia athari za tabia nchi kutokana na mradi wake wa bomba la mafuta kati ya Uganda na Tanzania, mawakili wake wamesema hapo jana.

Yakiongozwa na Darwin Climax Coalitions na Sea Shepherd France pamoja na mashirika mengine mawili, yanataka mradi huo kusitishwa.

Mawakili wa Mashirika hayo, wakiongozwa na William Bourdon, wamesema kesi hiyo imewasilishwa dhidi ya kampuni hiyo ya TotalEnergies, nchini Ufaransa tangu Septemba 22.

Katika kesi hiyo, mashirika hayo yanasema, ujenzi wa mradi huo, utasababisha uharibifu mazingira, mali na kusababisha maisha ya watu wa nchi hizo mbili.

Mbali na wanaharakati hao, Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linataka pia kusitishwa kwa ujenzi huo, wenye urefu wa Kilomita 1,445 kutoka Hoima nchini Uganda hadi kwenye Bandari ya Tanga nchini Tanzania, wenye thamani ya Dola Bilioni 10.

Licha ya shinikizo hizi, rais Yoweri Museveni ameapa kuwa ni lazima mradi huo uendelee, huku kampuni ya TotalEnergies ikisema watu zaidi ya Laki Moja, watakaothiriwa na mradi huo, wamelipwa fidia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live