Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashirika viwango EAC yaja kivingine

TBS EACfa130248428b 780x470 Mashirika viwango EAC yaja kivingine

Wed, 3 May 2023 Chanzo: Habarileo

MASHIRIKA ya viwango vya ubora wa bidhaa kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), yamejipanga kuhakikisha masuala ya bidhaa na vipimo yanakuwa sawa, husasan upimaji na magari yanayosafirisha mafuta.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha wakati wa mkutano wa 25 wa kujadili masuala ya viwango kwa nchi wanachama wa EAC, Mkurugenzi Udhibiti Ubora Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Lazaro Msasalaga, anasema mkutano huo wa siku tatu umejumuisha wakurugenzi wa viwango kutoka nchi za EAC ni muhimu kwa ajili ya kurahisisha ubora wa bidhaa na uhakika wa fursa za kujikwamua kiuchumi.

Anasema mashirika hayo yanakutana kupitia kamati za kitaalam katika masuala ya udhibiti ubora ikiwemo kupitisha viwango 69 za bidhaa chakula na vipodozi, ikiwemo viwango vitatu vinavyotoa maelekezo ya bidhaa husika na jinsi ya kuhifadhi.

“Hiki ni kikao muhimu na nchi ya Tanzania tutanufaika katika ubora wa viwango ikiwemo uwekaji wa maneno yanayoelezea bidhaa wanazotumia walaji zitaboresha vitu gani, ikiwemo viambata vya kilishe sanjari na ujumla wa kuweka maelezo ya aina mbalimbali katika bidhaa,” amesema.

Mkurugenzi wa Shirika la Ukaguzji wa Ubora wa Bidhaa kutoka nchini Kenya (KEBS), Bernard Njiraini, alisema mashirika hayo yanajadiliana viwango walivyokubaliana kwa pamoja, ili waweze kufanya biashara nchi mbalimbali kwa kupitisha bidhaa.

Meneja Upimaji Wakala wa Vipimo Tanzania, Magesa Biyani, anasisitiza masuala ya vipimo ni eneo muhimu kuhakikisha bidhaa na vipimo vinakua sahihi katika ufanyaji biashara kwa nchi za EAC hususan masuala ya upimaji katika magari yanayosafirisha mafuta, ambapo awali upimaji ulitofautina baina ya nchi na nchi, lakini pia wanatarajia kuanzisha kanuni itayoondoa vikwazo kwa wafanyabishara wanaosafirisha mafuta kwa nchi za EAC, ikiwemo ubora wa bidhaa

Chanzo: Habarileo