Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marufuku ununuzi wa Mafuta ya Urusi

Urusiiiii Marufuku ununuzi wa Mafuta ya Urusi

Mon, 9 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mataifa yenye uchumi mkubwa Duniani yanayounda Kundi la G7 yametoa kauli ya pamoja ya kupiga marufuku au kutonunua mafuta ya Urusi ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa vikwazo kwa taifa hilo lililoivamia Ukraine kijeshi tangu Februari 24, 2022.

Wamechukua maamuzi hayo baada ya mkutano wao wa mtandaoni jana Mei 8, 2022 kwa kuwa wanalenga moja ya chanzo kikubwa cha Urusi kuingiza mapato.

G7 ambayo inajumuisha Nchi a Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani imefanya kampeni hiyo ili kummaliza nguvu Rais wa Urusi, Vladimir Putin.

“Hii itakuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Rais Vladimir Putin na kumnyima mapato anayoyahitaji kufadhili vita vyake,” inaeleza kauli ya G7 baada ya mkutano kwa njia ya mtandao.

Baada ya mkutano wao huo pia walipata nafasi ya kuzungumza na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ambapo walimjulisha juu ya mipango yao hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live