Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marufuku meli za mizigo kupakia abiria

Meli Ya Mizigo1 Marufuku meli za mizigo kupakia abiria

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKALA wa Meli Tanzania (TASAC) imepiga marufuku abiria wanaotumia njia ya majini (bahari) kupanda vyombo vya kubeba mizigo na ambavyo havina leseni kwakufanya hivyo wanavunja sheria ikiwemo kukiuka sheria za usalama wa baharini.

Hayo ameyasema Ofisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga, Kapteni Christopher Shalua, wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya kumi ya biashara mkoa wa Tanga yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.

Amesema kuwa Kwa kutumia vyombo hivyo kusafiria sio tuu wanaweka maisha yao hatarini bali pia wanayaweka mashirika ya uokoaji katika hali ya shinikizo pindi pale ajali zinapotokea.

"Abiria lazima wazingatie itifaki zote za kiusalama kwa kupanda meli zilizo na leseni, “siyo kwa usalama wao tu, bali hata kwa usalama wa kila mtu aliye ndani ya vyombo hivyo,” amesema Kapt Shalua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live