Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marufuku kuchimba madini Geita bila leseni

Senyamule Ed Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule amewataka wananchi kufuata sheria za uchimbaji wa Madini ikiwa ni pamoja na kupata leseni ya uchimbaji kabla ya kuanza uchimbaji ili kuepusha migogoro kwenye jamii

RC Senyamule ameyasema hayo kwenye vijiji vya Buziku na Bwanga wilayani Chato alipofika kusikiliza kero za wananchi na kubaini kuwa kumekua na tabia ya wananchi kuanzisha machimbo isivyo halali kwenye maeneo yao na kusababisha migogoro.

"Ukigundua kuna madini sehemu usianze kuchimba kabla ya kupata leseni na zinapatikana kwa elfu hamsini tu na hakuna usumbufu wowote kwani tusipofanya hivyo tunakua hatujitendei haki sisi wenyewe maana mwingine akiwa na leseni anakua ndio mmiliki wa eneo hilo kiuchimbaji." - Mkuu wa Mkoa.

Aidha pia Senyamule akatumia wasaa huo kumtaka mratibu wa TASAF wilaya hiyo kufuatilia malalamiko ya wananchi ya kukosa uwezeshwaji na hali ya kwamba ni masikini pamoja kuwasisitiza maafisa Maendeleo wa kata kutoa elimu kwa wananchi juu ya uanzishwaji wa vikundi ili waweze kunufaika na mikopo ya halmashaur

Chanzo: www.tanzaniaweb.live