Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mark Zuckerberg ampiku Elon Musk kwa utajiri

Elon Musk Na Mark Zuckerberg Wapanga Kuzipiga Mark Zuckerberg ampiku Elon Musk kwa utajiri

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa orodha ya matajiri duniani iliyotolewa na Bloomberg siku ya Ijumaa inaonesha Mkurugenzi wa Kampuni ya Meta Mark Zuckerberg amempiku kwa mara ya kwanza Mkurugenzi wa Tesla, Bilionea Elon Musk.

Katika orodha hiyo Zuckerberg ameshika nafasi ya tatu kwa utajiri akiwa na utajiri wa dola bilioni 187 huku Elon Musk, akishuka hadi nafasi ya nne akiwa na utajiri wa dola bilioni 181.

Hii ni kwa mara ya kwanza kwa Zuckerberg kuingia katika tatu bora ya watu tajiri tangu mwaka 2020.

Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos anashika nafasi ya pili (dola bilioni 207) na Mkurugenzi Mtendaji wa LVMH Bernard Arnault yupo nafasi ya kwanza akiwa na utajiri wa ($223 bilioni).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live